31 Oktoba 2020 - 14:40
Mahathir Muhammad: Waislamu wana haki ya kuiadhibu Ufaransa

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia ameashiria mauaji ya umati ya huko nyuma yaliyofanywa na Ufaransa na kusema kuwa, Waislamu wana haki ya kukasirika na kuiadhibu Ufaransa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mahathir Muhammad amesisitiza kuwa, yeye anaamini suala la uhuru wa kujieleza lakini, hilo halipaswi kutumiwa kwa ajili ya kuwavunjia heshima watu wengine na kuonyesha vitendo vya utovu wa adabu dhidi ya matukufu yao.

Mwanasiasa huyo mkongwe wa Malaysia ameashiria mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Wafaransa huko nyuma na kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, bila shaka Waislamu wana haki ya kukasirika na kuchukua hatua za kuaidhibu Ufaransa.

Hata hivyo muda mchache baada ya Mahathir kuandika ujumbe huo, mtandao wa Twitter ulifuta ujumbe huo kwa madai kwamba, unakiuka sheria zake.

Mahathiir Muhammad ameashiria pia matamshhi ya hivi karibuni ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na kumtaja kiongozi huyo kama mwanagenzi.

Wakati huo huo, radiamali mbalimbali na matamko tofauti ya kulaani hatua ya Rais wa Ufaransa ya kutetea vitendo vya kuvunjiwa heshima Bwana mtume SAW yameendelea kutolewa na shakhsia na viongozi  mbalimbali wa kidini na kisiasa.

Maulama wa Kishia nchini Afghanistan wametoa tamko la kulaani hatua hiyo ya Rais wa ufaransa na kueleza kwamba, ni hujuma ya wazi dhidi ya Waislamu.

Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameelezaa kusikitishwa kwake na kitendo cha Rais wa Ufaransa na kukosoa vikali kuhalalisha ufidhuli na utovu wa adabu dhidi ya Mtume SAW kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

342/